Ujauzito ni hali ya mja kuwa mzito kutokana na mimba. Mimba ni mtoto wa mamalia ambaye anakua katika tumbo la uzazi la mama yake hadi azaliwe. pia Mimba ni neno linalotumiwa kuelezea kipindi ambacho kijusi hukua ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke. Kwa kawaida mimba hudumu takriban wiki 40, au zaidi ya miezi 9, kama inavyopimwa kuanzia hedhi ya mwisho hadi kujifungua. Watoa huduma za afya hurejelea sehemu tatu za ujauzito, zinazoitwa trimesters Dalili za ujauzito 1. Kukosa hedhi. Hii ni dalili kuu za ujauzito japo mwanamke anaweza kukosa hedhi kwa sababu ya maradhi, msongo wa mawazo, aina ya vyakula anavyokula pamoja na matumizi ya dawa mbalimbali. 2. Kutokwa na damu kidogo. Hii hutokea kwa baadhi ya wanawake haswaa siku 6 hadi 12 wakati wa upandikizaji wa yai lililorutubishwa. 3.Matiti kuvimba. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni na hutokea wiki ya kwanza hadi ya pili ya ujauzito. 4. Uchovu. Hii ni kwa sababu mwili progesterone ili kuchochea uzalishaji wa homoni za maziwa...