Ujauzito ni hali ya mja kuwa mzito kutokana na mimba.
Mimba ni mtoto wa mamalia ambaye anakua katika tumbo la uzazi la mama yake hadi azaliwe.
pia
Mimba ni neno linalotumiwa kuelezea kipindi ambacho kijusi hukua ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke.
Kwa kawaida mimba hudumu takriban wiki 40, au zaidi ya miezi 9, kama inavyopimwa kuanzia hedhi ya mwisho hadi kujifungua. Watoa huduma za afya hurejelea sehemu tatu za ujauzito, zinazoitwa trimesters
Dalili za ujauzito
1. Kukosa hedhi. Hii ni dalili kuu za ujauzito japo mwanamke anaweza kukosa hedhi kwa sababu ya maradhi, msongo wa mawazo, aina ya vyakula anavyokula pamoja na matumizi ya dawa mbalimbali.
2. Kutokwa na damu kidogo. Hii hutokea kwa baadhi ya wanawake haswaa siku 6 hadi 12 wakati wa upandikizaji wa yai lililorutubishwa.
3.Matiti kuvimba. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni na hutokea wiki ya kwanza hadi ya pili ya ujauzito.
4. Uchovu. Hii ni kwa sababu mwili progesterone ili kuchochea uzalishaji wa homoni za maziwa kwenye matiti pia ongezeko la msukumo wa damu ili kusafirisha oksijeni na virutubisho kwa kijusi. Hii humsababisha mama mjamzito kuchoka
5.maumivu ya kichwa kwa sababu ya ongezeko la uzalishaji wa homoni.
6.kichefu chefu na kutapika. Hii hujulikana kama ugonjwa wa asubuhi (morning sickness) na hutokea wiki ya 2 hadi 8 tangu mimba kutungwa.
7.Tamaa ya chakula au chuki.
8.Mhemko wa hisia .
9. Kukojoa mara kwa mara. Hii ni kwa sababu Human Chorionic Gonadotropin (HCG) huongeza mtiririko wa damu eneo la nyonga (pelvis).
Kipimo cha ujauzito;
Ni kipimo ambacho kinaweza kubainisha kama una mimba kwa kuchunguza homoni ya Human Chorionic Gonadotropin (HCG) katika sampuli ya mkojo au damu.
Viwango vya HCG hupanda kwa kasi katika wiki kumi za kwanza baada ya yai lililorutubishwa kupandikizwa.
(a) Vipimo vya ujauzito wa mkojo:
Hizi ni sahihi zaidi zinapofanywa wiki moja au mbili baada ya kukosa hedhi.
Ikiwa utapima mkojo mara tu baada ya kuwa mjamzito, kipimo kinaweza kuonyesha kuwa wewe si mjamzito hata kama una mimba. Hii ni kwa sababu mwili wako unaweza kuwa haujatoa HCG ya kutosha.
Unaweza kupimwa mkojo wa HCG hospitalini au nyumbani ukitumia kifaa cha kupima ujauzito nyumbani.
(b) Vipimo vya damu vya ujauzito
Vipimo hivi vinapaswa kufanywa hospitalini au maabara. Vipimo hivi vinaweza kugundua kiwango kidogo sana cha HCG, na kuwaruhusu kuamua ikiwa una mjamzito kabla ya kukosa hedhi. Hata hivyo, vipimo vya damu vya hCG havitumiwi sana kugundua ujauzito. Hii ni kwa sababu vipimo vya mkojo vina gharama ya chini, sahihi zaidi, na hutoa matokeo haraka kuliko kupima damu.
Matokeo yanaweza kuchukua saa kadhaa hadi siku kadhaa.
Lishe ya Mama Mjamzito
Lishe bora wakati wa ujauzito humpatia mama virutubishi muhimu.
Lishe bora huimarisha afya ya mama na humsaidia mtoto kukua vizuri kimwili na kiakili.
Ukosefu wa lishe bora wakati wa ujauzito huweza kusababisha mama kutoongezeka uzito kama inavyotakiwa na hivyo kukosa nguvu, upungufu wa damu (anaemia) wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ambao huweza kusababisha hata kifo, uwezekano wa mimba kuharibika, mtoto kufia tumboni, kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu (low birth weight), kuzaa mtoto njiti (still birth) au kuzaa mtoto mfu.
Mambo ya kuzingatia;
Kula milo minne kwa siku na asusa au vitafunwa mara nyingi kadri uwezavyo hii itakuwezesha kuupa mwili nguvu na lishe ya kutosha kwa ajili yako na mtoto anayekua tumboni.
Hakikisha mlo wako unakuwa na vyakula mchanganyiko vinavyopatikana katika jamii. Asusa au vitafunwa vinaweza kuwa vitu kama vile mahindi ya kuchoma au kuchemsha, kikombe cha maziwa, viazi, mayai, karanga, matunda n.k.
Kuepuka kunywa kahawa au chai wakati wa mlo kwani huingiliana na ufyonzwaji wa virutubisho katika mwili.
Kumeza vidonge vya kuongeza damu Ferrous and Folic acid tablets (FEFO) kila siku kwa kipindi chote cha ujauzito.
Vyakula vya asili ya wanyama huongeza damu kwa haraka zaidi.
Kula matunda ya aina mbali mbali yanayopatikana kwa msimu huo na mbogamboga kwa wingi kila siku
Kula vyakula vilivyoongezwa virutubishi, kwa mfano unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kupikia.
Kutumia chumvi yenye madini joto wakati wote.
Kunywa maji ya kutosha kila siku (angalau glasi 8 au lita 1.5). unaweza ukaongeza ladha kwa kuweka limau au ndimu.
Kujikinga na Malaria kwa kutumia vyandarua vilivyowekwa viwatilifu na kutumia dawa za kuzuia malaria na minyoo kama inavyoshauriwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Kujikinga na maambukizi ya magonjwa na virusi vya UKIMWI
Kuepuka utumiaji wa sigara na pombe kwani inaathiri matumizi ya virutubishi na afya ya mama na mtoto.
Kuanza kliniki mapema mara tu ya kujihisi mjamzito na uendelee kuhudhuria ili kupata huduma na ushauri zaidi utakaoboresha lishe na afya kwa ujumla.
Naitwa Amos ni mtaalamu wa afya karibu sana tujifunze pamoja.
Karibu kwa maswali yote pamoja na tiba ya magonjwa mbalimbali
Email; amosmasoud02@gmail.com






Comments
Post a Comment